TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara,
Idara zinazojitegemea, Taasisi za Serikali, na Mamlaka ya Serikali za
Mitaa (MDA’s na LGA’s), Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Mkemia Mkuu wa
Serikali (GCLA) na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) anatarajia
kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi
watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
1. Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k.
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, Sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
5. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
6. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyia usaili.
7. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
8. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
9. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.
10. Kila mwombaji aliyeitwa katika usaili anaelekezwa kukariri Jopo la usaili alilopangiwa kama ilivyoanishwa kwenye tangazo hili.
Kufungua tangazo na Orodha ya majina(pdf) BOFYA HAPA
0 Comments